Rais Jakaya Kikwete akimpongeza mama Agnes Msavi mara baada ya kumtwisha ndoo ya maji kuashiria ukombozi kwa mwanamke kutokana na kukamilika kwa mradi huo.
Warembo wa kimasia wakiwmlaki Rais Jakaya kikwete huku wakiwa wameshikilia bendera za taifa alipowasili katika kijiji cha Itunundu.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamanda wa vijana mkoani Iringa Salim "Sas" Abri mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Askofu wa Dayosisi ya Ruaha Joseph Mgomi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa leo mchana, kushoto ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Ruaha Dornald Mtetemela.
Rais Jakaya Kikwete akiwatunza wasanii wa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati alipowasili mjini Iringa leo.
Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma kushoto mara baada ya kuwasili mjini Iringa leo, kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Grayson Rwenge.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Evarist Mangalla katika uwanja wa ndege wa Nduli.
Rais Jakaya Kikwete akipungia wananchi mkono mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa leo mchana.
Ndege iliyomleta Rais Jakaya Kikwete ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Nduli jana mchanaChanzo:Full Shangwe
0 comments:
Post a Comment